Duration 3:31

USAFIRISHAJI WA NYAMA KUTOKA MWANZA KWENDA DUBAI KWA SIKU MOJA

3 333 watched
0
16
Published 5 Jan 2019

Wafanyabiashara mkoani Mwanza wameendelea kutumia shirika la ndege Tanzania ATCL kusafirisha bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA ameshuhudia usafirishaji wa tani mbili za nyama ya mbuzi kutoka kiwanda cha CHOBO INVESTIMENT cha mkoani Mwanza kwenda nchini DUBAI kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam. Kiwanda cha Nyama cha CHOBO INVESTMENT cha Mkoani Mwanza kimesafirisha zaidi ya tani 2 ya nyama ya mbuzi kwa kutumia shirika la Ndege Tanzania ATCL kwenda nchini DUBAI kupitia uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Usafirishaji huo umeshuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA ambaye amesema kuwa hii ndiyo faida ya kufufa shirika hilo na sasa kila mwananchi ni jukumu lake la kutumia fursa ya kujiimarisha kiuchumi. Uwepo wa ndege za ATC nchini ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza na nchi nzima kwa ujumla kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi. Mkurugenzi wa kiwanda cha chobo investiment JOHN CHOBO amesema lengo la kampuni ni kuongeza uzalishaji hivyo wamejipanga kutoa elimu kwa wafugaji wa kanda ya ziwa huku mnunuzi wa nyama hizo ISSA AL-FALAS …kutoka nchini DUBAI akipongeza serikali kwa uwepo wa ndege hizo.

Category

Show more

Comments - 6